Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amempa masaa 24 beki wa klabu hiyo Gadiel Michael awe amesaini mkataba mpya baada ya ule wa awali wa miaka miwili kuwa umemalizika.
Mwenyekiti huyo msomi amefikia hatua hiyo baada ya beki huyo kuwa msumbufu kila anapoitwa kuja kusaini licha ya kuwa stahiki zake katika mkataba kuwa zimetimizwa.
Yanga wameoneshwa kuchoshwa na usumbufu wanaoupata kutoka kwa beki huyo ambaye amekuwa akiwapiga chenga kuja kutia saini licha ya kuwa wamekubaliana kila kitu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Gadiel alisajiliwa na Yanga akitokea Azam Fc alikocheza kwa misimu kadhaa baada ya kuwa amepandishwa katika timu ya wakubwa akitokea timu ya vijana ya timu hiyo.