Mabao matatu ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema yalitosha kuwaondosha Psg katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya mchezo uliofanyika jijini Madrid.
Paris st.German wakiwa mbele kwa bao 1 waliloshinda katika mechi ya awali jijini Paris walihitaji sare ya aina yeyote kuweza kufuzu hatua ya robo fainali lakini ndoto hizo ziliyeyuka kipindi cha pili baada ya Benzema kufunga mabao matatu kipindi na kuwatoa Psg katika michuano hiyo licha ya kutangulia kufunga dakika ya 39 kupitia kwa Kylian Mbappe.
Mshambuliaji huyo mkongwe Mfaransa, Karim Benzema alifunga katika dakika za 61,76 na 78 baada ya PSG kutangulia kwa bao la mshambuliaji Mfaransa mwenzake na kuzua shangwe kwa mashabiki wa Real Madrid uwanjani hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na ushindi huo Real Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa 16 Bora Ufaransa kwa bao la Mbappe.