Kwa mara nyingine tena, bodi ya ligi kuu nchini imefanikisha kutoa uzinduzi wa msimu wa NBC Premier League wa 2025–2026 kwa aina yake baada ya kuitangaza ratiba rasmi ya michuano ya ligi kuu nchini leo jumaa tarehe 29 Agosti 2025 .
Kwa mujibu wa ratiba hiyo itakayoanza na mechi ya Ngao ya jamii (Community Shield) kati ya Wakongwe wa Ligi Kuu Tanzania, Young Africans (Yanga) na Simba Sc ambayo itafanyika kama maandalizi rasmi ya msimu mpya.
Mchezo huo ni mchezo unaochanganya heshima na ushindani, unatarajiwa kuchezwa tarehe 16 Septemba 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam .
Ratiba Kamili ya NBC Premier League 2025–2026
Ratiba inaonyesha kuwa msimu utachezwa kuanzia 17 Septemba 2025 hadi 23 Mei 2026 . Bodi ya ligi imetangaza mechi mbalimbali katika tovuti rasmi ya ligi kuu, ikionyesha muendelezo wa mechi kwa kipindi cha miezi kadhaa ijayo huku pia baadhi ya michezo itapangiwa viwanja kadri ratiba itakavyokua ikiendelea.
Hivi hapa kuna vipengele muhimu:
Msimu unanogeshwa kwa mechi za ligi kuanzia mwanzoni mwa msimu hadi majuma ya mwisho ya Mei 2026.
Ukusanyaji wa timu, mikusanyiko ya mechi za nyumbani na ugenini, na muda uliowekwa wa kucheza kila kitu kimewekwa kwa uwazi.
Mechi Inayosubiriwa kwa Hamu Zaidi: Simba vs Young Africans (Yanga)
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mchezo wa Kariakoo Derby baina ya Simba na Yanga ndio uliowekwa rasmi kwenye ratiba ya ligi. Tarehe iliyopangiwa ni 14 Desemba 2025, ambapo Yanga itakuwa nyumbani dhidi ya Simba SC . Hii ni mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote mbili, ikiwa ni moja ya michezo yenye msisimko zaidi katika soka la Tanzania.
Muhtasari wa Mambo Muhimu Katika Ratiba
- Uzinduzi wa Msimu 29 Agosti 2025 Bodi ya ligi imetangaza rasmi ratiba
- Community Shield 16 Septemba 2025 Young Africans vs Simba SC (jiji Dar es Salaam)
- Msimu wa Ligi Kuu kuanza rasmi 17 Septemba 2025 mpaka 23 Mei 2026.
- Derbi la Kariakoo (Yanga vs Simba) kuchezwa 14 Desemba 2025 ambapo hii ni Mechi kali inayoongozwa kwa hamasa kubwa
Sehemu ya Ratiba: Mechi za Mwanzo
Kwa msimu huu, baadhi ya mechi za ufunguzi zina oneshwa kwenye tovuti ya Ligi Kuu (ligikuu.co.tz). Hizi zitakuletea mwanga wa awali wa jinsi mechi zipo kuanzia mwanzo wa msimu:
17 Septemba 2025:KMC FC vs Dodoma Jiji (KMC Complex, Dar es Salaam) Coastal Union vs Tanzania Prisons, Fountain Gate vs Mbeya City, Mashujaa FC vs JKT Tanzania.