Home Soka Boko Aula Stars Chan

Boko Aula Stars Chan

by Dennis Msotwa
0 comments

Kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars Ettiene Ndayiragije amemteua mshambualiaji wa Simba sc John Boko kuwa nahodha wa kikosi hicho kuelekea katika mechi ya mtoano dhidi ya Kenya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani(Chan).

Mechi hizo zitakazochezwa julai 28 jijini Dar es salaam na marudiano itachezwa nchini Kenya Augusti 4,Mshambuliaji huyo mrefu atasaidiwa na Juma Kaseja,Erasto Nyoni na beki wa Yanga Kelvin Yondani ili kuhakikisha timu ya taifa inashinda michezo hiyo miwili muhimu.

Ettiene Ndayiragije ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa muda baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike kutimuliwa kutokana na kufanya vibaya katika michuano ya Afcon iliyofanyika nchini Misri ambapo Tanzania ilishiriki kwa mara ya pili baada ya miaka 39.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited