Timu ya Simba sc leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya manispaa ya Kinondoni(Kmc) katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Mo Simba Arena bunju jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo wenye lengo la kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara Kmc ilikua ya kwanza kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa Charles Ilanfya lakini bao hilo halikudumu baada ya Simba kusawazisha kupitia kwa John Boko aliyefunga bao jingine dakika ya 73 kabla ya Ibrahim Ajib kufunga bao la mwisho dakika ya 88.
Simba hivi leo imecheza michezo miwili ya kirafiki ambapo asubuhi iliilaza Transit Camp mabao 4-2 na jioni kushinda mabao 3-1 dhidi ya KMC.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.