Home Soka Brazil vs Argentina yaarishwa kisa Covid-19

Brazil vs Argentina yaarishwa kisa Covid-19

by Dennis Msotwa
0 comments

Mchezo wa kufuzu kombe la dunia Qatar 2022 ukanda wa Amerika ya Kusini kati ya Brazil mwenyeji dhidi ya Argentina umelazimika kuahirishwa dakika ya tano tu tangu kuanza chanzo kikitajwa kuwa ni Uviko-19.

Maafisa wa afya nchini Brazil waliingia uwanjani dakika ya tano ya mchezo kuwatoa nje wachezaji wanne wa Argentina wanaocheza soka lao nchini England ambao ni golikipa Emi Martinez,beki Christian Romero na viungo Lo Celso na Emi Buendia wakidai kuwa wachezaji hao wamekiuka masharti ya Uviko-19 ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa sheria za Uviko-19 za Brazil wachezaji hao walitakiwa kukaa karantini siku 14 kabla ya kujihusisha na shughuli yoyote lakini hawakufanya hivyo.Hata hivyo hatua hiyo imewashtua Argentina na wapenzi wa soka dunia kwani maafisa hao walitakiwa kuchukua hatua hiyo pindi tu wachezaji hao walipoingia Brazil na sio kuwatoa katikati ya mchezo.

banner

Wachezaji wa Argentina walitoka nje baada ya maafisa hao kuingia uwanjani kuwatoa wachezaji hao na baada ya sintofahamu ya muda mrefu mwamuzi wa mchezo huo alihairisha mchezo huo,FIFA itakusanya itakusanya ushahidi toka pande zote kabla ya kutangaza hatua zilizochukuliwa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited