Afisa Habari-Yanga Hassan Bumbuli ameshinda rufaa ya kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa miaka mitatu hukumu ambayo ilitolewa na TFF ikielezwa Bumbuli amekaidi uamuzi wa Kamati ya Maadili dhidi yake.
Taarifa za kushinda kwa rufaa ya Afisa huyo zimesambaa hivi leo katika mitandao mbalimbali huku bado taarifa rasmi kutoka shirikisho la soka nchini TFF ikiwa bado haijatoka.
Kwa maana hiyo, Bumbuli yupo huru kuendelea na shughuli za soka ikiwa ni pamoja na kuitumikia klabu yake ya Yanga.