Shirikisho la soka nchini Tanzania Tff limesimamisha shughuli zote za michezo ya soka nchini kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli kilichotokea jana jioni kufuatia kusumbuliwa na maradhi ya moyo.
Awali baada ya taarifa kusambaa kufuatia kutoonekana hadharani kwa muda mrefu huku shughuli zikiendelea kama ilivyo kawaida lakini kufuatia tangazo rasmi la serikali kuhusu msiba huo kumesababisha shughuli za michezo ya soka kusimamishwa na shirikisho hilo.
Moja ya ratiba iliyoathirika ni mechi ya kirafiki baina ya timu ya taifa ya Tanzania iliyokua icheze mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya machi 18,ratiba hiyo imeahirishwa japo timu hiyo itaendelea kuweka kambi nchini Kenya.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Taarifa rasmi kutoka Tff inaonyesha kuwa michezo mbalimbali ya soka itasimama kwa muda wa wiki mbili kupisha kipindi cha maombolezo.