Site icon Sports Leo

Camavinga aingia rada za Man Utd

Mchezaji kinda wa Kifaransa Eduardo Camavinga yupo katika mipango ya kutakiwa na mashetani wekundu Manchester united katika dirisha hili la majira ya joto pindi tu itakapokamilisha dili la Jadon Sancho.

Camavinga mwenye umri wa miaka 18 anayekipiga katika klabu ya Rennes ya Ufaransa anatajwa kuwa mrithi wa Mfaransa mwenzake Paul Pogba anayehusishwa kutakiwa na matajiri PSG ya Ufaransa. Mkataba wa Pogba unatarajiwa kumalizika mwaka 2022, hivyo Man Utd wanahisi huenda wakampoteza baada ya kusuasua kwa mazungumzo ya mkataba mpya.

Man Utd itakabiliwa na upinzani kutoka katika klabu za PSG, Real Madrid na Arsenal katika kuwania saini ya kiungo huyo mahiri.

Exit mobile version