Cletous Chama ni habari nyingine nchini Tanzania baada ya kutumia dakika 30 kuimaliza timu ya Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.
Polisi waliwamudu Simba sc kipindi cha kwanza na kusababisha kwenda mapumziko wakiwa suluhu lakini mabadiliko ya mwalimu Sven Vandebroek ya kuwaingiza John Boko na Cletous Chama yalileta matunda dakika ya 65 baada ya Chama kufunga la uongozi akimchambua kipa wa Polisi Tanzania.
Dakika ya 90 Chama tena alimtungua kipa wa Polisi Tanzania baada ya kuachwa kuambaa na mpira bila kubughudhiwa na kuimaliza mechi kwa ushindi wa 2-0 na kuifanya Simba sc kufikisha alama 26 za msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.