Site icon Sports Leo

Chamazi Kufanyiwa Marekebisho Makubwa

Uongozi wa timu ya Azam fc umeamua kuufanyia marekebisho makubwa uwanja wa Chamazi Complex ili kuendana na hadhi ya viwanja vikubwa duniani kama Alliance Arena wa Bayern Munich.

Akiongea na waandishi wa habari Mhandisi mkuu wa kampuni hiyo alisema kuwa marekebosho hayo ni matunda ya ziara yake aliyoifanya barani ulaya kutembelea viwanja vikubwa.

“Tukaona ni vema tubadilishe taa, tayari ilikuwa ipo kwenye malengo yetu ilikuwa ni plan ya mwaka 2019 hadi 2021, plan ilikuwa tuanze na sehemu ya kuchezea, kisha tutakuja taa, kisha tutakuja na kitu kingine kipya naweza kusema kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki tunakitambulisha siku ya leo kwa kuweka mabango ya matangazo ya kielektroniki kwenye uwanja wetu.
“Uwekaji wa taa hizi unaendelea, tumeanza rasmi wiki iliyopita kuondoa taa za zamani na tumetoka kwenye mfumo wa taa za kizamani tunaenda kwenye mfumo wa taa za kisasa zaidi ambazo zinatumika kwenye viwanja vingi duniani, ambazo mwanga wake ni mweupe yaani unavyokuwa unacheza usiku basi unajisikia kama unacheza mchana bila kuona kivuli au kitu chochote kile,” aliongeza Mhandisi Ndozero.

Exit mobile version