Mabingwa wa klabu bingwa Ulaya Chelsea wamefanikiwa kuchukua kombe la Uefa super cup baada ya kuwafunga manyambizi wa njano klabu ya soka ya Villareal kutoka Hispania kwa changamoto ya mikwaju ya penati 7-6.
Timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1 ndani ya dakika na kupelekea mchezo kwenda dakika 30 za nyongeza ambapo pia matokeo yalikuwa suluhu ya 0-0.
Chelsea ilijipatia goli lake kunako dakika ya 27 kupitia Hakim Ziyech akimalizia pasi ya Kai Havertz,huku Villareal ikisawazisha dakika ya 81 kupitia kwa Gerard Moreno.
Golikipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga akiokoa mikwaju miwili ya penati na kuipa ushindi timu yake.