Chelsea wamethibitisha kuwa wamefikia makubaliano na klabu ya RB Leipzig juu ya uhamisho wa mshambuliaji Timo Werner.
Werner amesaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya €170,000 kwa wiki, na Mjerumani huyo atawasili Stamford Bridge mnamo mwezi Julai akisajiliwa kwa ada ya pauni milioni 47.5.
Blues imethibitisha kwamba straika huyo ataendelea kubaki na klabu yake ya sasa hadi mwisho wa msimu huu wa Bundesliga, lakini ataungana na timu yake mpya kabla ya msimu wa 2019/20 wa England kumalizika.
Akiongea na wavuti rasmi ya Chelsea, Werner amesema: “Nimefurahi kusaini Chelsea, ninajivunia sana kujiunga na klabu kubwa kama hii.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Ninashukuru pia klabu yangu ya RB Leipzig, mashabiki, kwa miaka minne bora kabisa nikiwa hapa. Itabaki moyoni mwangu milele. Najipanga na msimu ujao na wachezaji wenzangu wa timu mpya, meneja wangu na bila shaka mashabiki wa Chelsea “Kwa pamoja naona tutakuwa na mafanikio makubwa kwa kipindi kijacho.”
Werner moja ya maforwad wenye uwezo wa kucheza mahali popote kwenye safu ya ushambuliaji, hadi sasa msimu huu amefunga mabao 32 na kutoa asssists 13 katika mechi 43 akiwa msaada mkubwa kwa RB Leipzing inayoshika nafasi ya 3 ktk Ligi na imefuzu Robo fainali ya Champions League.