Shirikisho la soka barani Afrika CAF limebadilisha sheria ya upimaji wa vipimo vya covid katika michezo kutokana na kuongezeka kwa malalamiko kwa baadhi ya timu nchini kuhusu uhalali wa majibu.
Awali timu za nyumbani zilihusika katika kupima ugonjwa huo kwa timu husika na timu ngeni. Kuanzia wikiendi hii CAF wataweka wawakilishi wao na kupima ugonjwa huo.
Lengo kubwa la kubadili utaratibu huo ni kuongeza ufanisi na usahihi wa majibu ili kuhakikisha timu ngeni hazionewa kwa kisingizio cha baadhi ya mastaa wana Covid ili kuwadhoofisha.