Ron Smith ambae ni Baba Mzazi wa kocha wa Aston Villa Dean Smith afariki Dunia hii leo baada ya kuugua Corona kwa muda wa wiki nne huku pia akisumbuliwa na maradhi mengine.
Dean Smith ambaye ni kocha wa mtanzana Mbwana Samata amefiwa na baba yake huyo mwenye umri wa miaka 79 alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu miezi sita iliyopita na alikutwa na Corona wiki nne zilizopita ugonjwa uliochukua uhai wake.
Ron Smith alikuwa shabiki mkubwa na mlinzi katika uwanja wa Ston Villa (Villa Park) kwa kipindi kirefu alikuwa ni miongoni mwa mashabiki walioshuhudia Aston Villa wakitwaa ubingwa wa Ulaya 1982.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.