Mabosi wa timu ya Dodoma Jiji Fc wamefikia makubaliano na aliyekuwa Kocha mkuu wa Singida Black Stars, Mecky Maxime kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao wa ligi kuu nchini unaotarajiwa kuanza mwezi Augusti.
Hatua hiyo inafuatia baada ya Maxime kuachana na Singida BS (zamani Ihefu) kumpisha kocha wa zamani wa Simba na AFC Leopards, Patrick Aussems ambaye amefikia makubaliano ya kukinoa kikosi hicho kuanzia msimu ujao.
Maxime ambaye ni kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar na Kagera Sugar amesaini mkataba wa miaka miwili ingawa kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja huku aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Mkenya, Francis Baraza akitimuliwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha huyo ni moja ya makocha bora wazawa akijulikana kwa misimamo yake pamoja na kufahamu jinsi ya kuishi na wachezaji wazawa ili kulinda viwango vyao ambavyo mara nyingi huporomoka kutokana na kukosa nidhamu ya mazoezi.