Klabu za Chelsea na Inter Milan zimefikia makubaliano ya kuuziana mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku kwa ada ya takriban i Euro milion 115.
Mchezaji huyo mamefanywa vipimo vya afya jijini Milan Italia na amesafiri kwenda London Uingereza kusaini mkataba wenye thamani ya Euro milioni 12 kwa mwaka na kutambulishwa rasmi ndani ya wiki hii.
Lukaku anakuwa usajili ghali zaidi katika historia ya klabu ya Chelsea na anarejea baada ya kuondoka darajani mwaka 2014.