Baada ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi simba SC, Mo Dewji kudai mpango wa mabadiliko wa Klabu ya simba SC inakwamishwa na FCC baada ya kuagizwa Kuanza upya kwa mchakato huo, Mkurugenzi wa FCC Dr.John Mduma amesema FCC hawawezi kuizungumzia Kesi ambayo bado haijatolewa maamuzi.
“Hatuwezi kuizungumzia Kesi ambayo maamuzi yake bado hayajatoka mana tume ya Ushindani (FCC) ni kama mahakama ya mwanzo kwenye Ushindani kwa hiyo hatuwezi kuizungumzia Kesi ambayo haijaamuliwa kwenye vyombo vya Habari”. – Dr.John Mduma Mkurugenzi FCC.
Cc:Clouds Fm