Shirikisho la mpira wa miguu duniani(FIFA) limefungua rasmi uchunguzi wa wazi juu ya madai ya timu ya Taifa ya Afrika Kusini juu ya penati ya utata waliyopewa Ghana katika mchezo wa kufuzu hatua za mtoano kutinga kombe la dunia Qatar 2022.
Chama cha soka Afrika Kusini kilituma kilituma barua ya malalamiko juu ya mwamuzi Maguette Ndiaye aliyewzawadia penati Ghana na kuwapa goli pekee la mchezo lililowawezesha kutinga hatua ya kumi bora.
Baada ya kupokea malalamiko hayo FIFA imeyajubali na kuanza uchunguzi mara moja.
Katika mchezo huo mchezaji wa Ghana Daniel Amartey alijiangusha ndani ya eneo la kumi na nane wakati wa kugomea mpira wa kona dakika ya 33,hata hivyo mgusano kati yake na beki Rushine de Reuck ulikua ni mdogo sana ambao kikanua za soka haukupaswa kuwa ni adhabu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Endapo FIFA wakijiridhisha baada ya uchunguzi kuwa ni kweli maamuzi ya mwamuzi Ndiaye yalikuwa na utata basi kuna uwezekano mkubwa mchezo huo kurudiwa.