Site icon Sports Leo

Fifa Yamtambua Sasi

Hery Sasii ni miongoni mwa waamuzi 17 walioteuliwa kuvaa beji za Shirikisho la Soka la kimataifa (FIFA) mwakani.

Taarifa ya waamuzi hao imetolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuwataja wengine kwa waamuzi wa kati kuwa ni Florentina Zablon, Jonesia Rukyaa, Martin Saanya, Mfaume Nassoro na Ramadhan Kayoko.

Waamuzi wasaidizi ni Abdulaziz Ally, Ferdinand Chacha, Frank Komba, Hellen Mduma, Janet Balama, Kassim Mpanga, Mbaraka Haule, Mohamed Mkono na Soud Lila.

Siku za karibuni mwamuzi Henry Sasi amekua na maamuzi tata katika michezo aliyochezesha kiasi cha kuwatia hofu mashabiki kuhusu kiwango cha mwamuzi huyo hasa baada ya kuipa Simba sc penati ambayo haikua sahihi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kmc.

Credit:Dominick Salamba

Exit mobile version