Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Fiston Abdoul Razack, ametimka klabuni baada ya mkataba wake wa miezi sita kumalizika Julai 12, 2021 na huku kukiwa hakuna dalili za kuongezewa mkataba mpya.
mchezaji huyo alijiunga na Yanga sc chini ya kocha Cedrick Kaze mwezi januari mwaka huu kwa mkataba mfupi wa miezi sita tu,ameifungia Yanga bao moja Ligi Kuu Bara na bao lingine Kombe la FA ambapo Jumla ni mabao mawili katika michezo yote aliyocheza ya kimashindano na kirafiki.
Yanga sc haijaonyesha nia ya kuendelea na mshambuliaji huyo kutokana na kushindwa kulishawishi benchi la ufundi chini ya kocha Mohamed Nasredine Nabi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.