Site icon Sports Leo

Fraga Anarejea..

Kiungo mkabaji raia wa Brazil Gerson Fraga Vieira yupo mbioni kurejea katika klabu ya Simba sc baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Kiungo huyo mkabaji alipata jeraha la goti wakati akiitumikia klabu hiyo ambapo alihitaji muda mrefu wa matibabu hivyo kuilazimu klabu hiyo kukaa chini kuangalia namna ya kuziba nafasi yake ambapo walikubaliana kuvunja mkataba ili apate matibabu huku akirejea nyumbani kwao nchini Brazil.

Sasa kiungo huyo tayari amepona na hivi karibuni aliweka maneno katika mtandao wake wa instagram akisema kuwa ”Tutaonana si mrefu” hali iliyowafanya wemgi kuamini kuwa staa huyo aliyecheza na Neymar na Coutinho katika kikosi cha vijana timu ya Taifa ya Brazil kuwa anaweza kurejea nchini kujiunga na klabu yake hiyo.

Exit mobile version