Klabu ya Everton ya nchini England, imethibitisha kuwa mchezaji wao Andre Gomes atafanyiwa upasuaji leo hii nchini humo.
Gomes alivunjika mguu wake wa kulia siku ya jana katika mchezo wa ligi dhidi ya timu ya Tottenham Hotspurs.
Katika mchezo huo, Heung Son wa Spurs alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, baada ya kumchezea rafu Gomes iliyompelekea kwenda kugongana na beki wa Spurs, Serge Aurier na kusababisha kuvunja mguu wake.
Mreno huyo alitolewa kwa msaada wa machela katika uwanja wa Godson Park, kabla ya kupelekwa katika hospital ya Aintree kwa matibabu na vipimo zaidi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Klabu yake ya zamani Barcelona imemtumia salamu za pole pamoja na mastaa mbalimbali duniani akiwemo Lucas Digne beki wa Barcelona ambaye walicheza wote Nou camp.