Unaambiwa tajiri wa klabu ya Yanga sc Gharib Said Mohamed anajiandaa kumwaga mamilioni ya pesa kama zawadi endapo timu hiyo itatwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuukosa kwa miaka karibuni mitano sasa.
Iko hivi baada ya kutwaa kombe la mapinduzi bilionea huyo alitoa zawadi ya milioni mia tatu kwa wachezaji ambapo sasa katika duru la pili la ligi kuu nchini amewaahidi zawadi nono endapo watatwaa ubingwa huku wakipandishiwa bonasi za mechi wanayoshinda mpaka milioni sabini za kitanzania.
Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimesema uwepo wa mamilioni hayo kumemfanya kocha kaze pamoja na benchi la ufundi na wachezaji wapambane kuhakikisha wanapata matokeo kila kukicha.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.