Home Soka Hakimi kutua PSG

Hakimi kutua PSG

by Sports Leo
0 comments

Beki wa kulia wa Inter Milan Achraf Hakimi anatarajia kujiunga na matajiri PSG ya Ufaransa baada ya makubaliano kufikiwa baina ya Inter Milan na PSG kuhusu ada ya mchezaji huyo.

Inter Milan itapokea kiasi cha euro milini 60 inayotarajiwa kupanda hadi kufikia euro milioni 70 hapo baadae. Makubaliano binafsi kati ya Hakimi na PSG yalishafikia tayari na anatarajiwa kusafiri hadi katika jiji la Paris kwa ajili ya vipimo vya afya.

Hakimi anaondoka Inter Milan baada ya msimu mmoja tu akishinda ubingwa wa seria A na klabu yake hiyo baada ya kujiunga nayo msimu uliopita akitokea Real Madrid kwa euro milioni 40. PSG imefanikiwa kumpata Hakimi baada ya kuipiku Chelsea katika mbio hizo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited