Uongozi wa Yanga kupitia kwa Ofisa Uhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz umesema hawajakata tamaa ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwani bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika michezo ijayo.
“Hatujakata tamaa. Tuendelee kupambana kwenye kila mchezo kwa kila namna, ibakie kuwa ni matokeo ya mpira na bahati ya siku yenyewe.”
“Hapa lengo letu ni moja tu, kuendelea kupambana hadi pumzi yetu ya mwisho, na tunaamini tutapata tunachokikusudia, na hicho sio kingine zaidi ya ubingwa wa Tanzania Bara ambao tumeukosa kwa misimu mitatu mfululizo,” alisema Nugaz
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.