Kiungo wa klabu ya Simba sc Fabrice Ngoma amewapa masharti viongozi wa klabu hiyo kusajili mastaa wa maana ili asalie kikosini humo na ikiwa vinginevyo basi anaweza kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Kiungo huyo inadaiwa ana ofa kutoka klabu za Pyramid Fc, Al Alhy na Raja Casablanca ambapo ameamua kusubiri mpaka mwishoni mwa msimu huu kuamua hatma yake kama ataondoka ama atasalia klabuni hapo licha ya kwamba ana mwaka mmoja umesalia katika mkataba wake.
“Alisema anataka kuona Simba SC inachukua mataji. Hivyo tutasajili wachezaji wenye moyo wa kujituma na uchungu na timu.” alidokeza kiongozi huyo na kuongeza huku akisisitiza anaona ndani ya kikosi hicho ameona wachezaji wachache wa kigeni ndio wenye moyo wa kuipambania timu jambo linalomuumiza kuona wakati anarejea mapumziko nchini kwao anakuwa hana furaha.”Kilisema chanzo chetu cha ndani ya klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.