Home Soka Hazard Wodini Miezi 3

Hazard Wodini Miezi 3

by Sports Leo
0 comments

Staa wa Real Madrid Eden Hazard atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu akiuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa enka jijini Dallas nchini Marekani.

Upasuaji huo uliofanyika katika hospitali ya The Carrell Clinic ulisimamiwa na Dkt. Eugene Curry na ulikua na mafanikio makubwa huku ikionyesha kuwa atahitaji miezi 2-3 kukaa sawa.

Taarifa kutoka katika klabu ya Real Madrid ilisomeka kuwa “Mchezaji wetu Eden Hazard amefanyiwa upasuaji leo (jana), Dallas katika mguu wake wa kulia,Upasuaji huo ulifuatiliwa kwa karibu sana na timu ya madaktari ya Real Madrid. Hazard anaendelea kuwa chini ya uangalizi madaktari hadi pale atakaporuhusiwa na kuanza safari ya kurudi kuwa fiti. Atakuwa nje kwa miezi miwili hadi mitatu. Daktari aliyemfanyia upasuaji anafanya kazi na timu ya Dallas Cowboys,” ilisema taarifa hiyo ya klabu ya Real Madrid.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited