Wachezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, Dennis Bergkamp na Patrick Vieira wamejiunga na mwanzilishi wa mtandao wa Spotify , bilionea Daniel Ek katika kuwaslisha ombi la kutaka kuinunua Arsenal.
Mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke hana lengo la kuiuza klabu hiyo , lakini zaidi ya mashabiki 1000 walifanya maandamano nje ya uwanja wa Emirates RYsiku ya Ijumaa wakimtaka kuiuza.
Arsenal ilikuwa imetangaza kwamba ni miongoni mwa klabu 12 zilizojiunga na Ligi ya Ulaya ya European Super league Jumapili iliopita Lakini saa 48 baadaye , walijiondoa na kuomba msamaha kwa mashabiki.