Site icon Sports Leo

Ibenge Aanza na Ushindi

Kocha mpya wa klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco Florent Ibenge ameanza mechi yake ya kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ittihad Tanger katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Morocco Botola Pro.

Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo akitokea As Vita Club ya DR Congo siku chache zilizopita ambapo alidumu klabuni hapo kwa miaka tisa akiipa mataji mbalimbali huku pia ikidaiwa analipwa zaidi ya shilingi milioni 100 kama mshahara.

Exit mobile version