Home Soka Injinia Amaliza Usajili wa Djuma Drc

Injinia Amaliza Usajili wa Djuma Drc

by Sports Leo
0 comments

Makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Yanga sc Injinia Hersi Said amelimaliza sakata la muda mrefu kuhusu usajili wa beki wa kulia wa klabu ya As Vita Shabani Djuma kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

Usajili huo ulikamilishwa jana jioni baada ya Injinia kusafiri kuelekea nchini Congo Drc ambapo alikamilisha dili hilo la staa huyo anayemilikiwa na As Meniema Union pamoja na As Vita.

Pia meneja wa mchezaji huyo ambaye anaishi nchini Ubelgiji akimiliki kampuni ya uwakala ya Pro Soccer Management naye alitua Congo kumaliza dili hilo na kuzima tetesi za kutakiwa na Azam Fc,Simba sc na timu za Magharibi mwa Afrika.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited