Kiungo mshambuliaji wa Everton na timu ya taifa ya Colombia amesafiri hadi katika nchi ya Qatar akiwa na wakala wake kwaajili ya mazungumzo ya kujiunga na Al Saad inayofundishwa na kiungo wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez.
James amepoteza namba katika kikosi cha kwanza tangu kutua kwa kocha Rafael Benitez ambaye anawatumia zaidi Demaray Gray na Aaron Townsend ambao wamesajiliwa msimu huu.
Mchezaji huyo alijiunga Everton mwaka 2020 kwa ushawishi wa aliyekua kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti,na alianza maisha yake vizuri katika klabu hiyo kabla ya majeraha kuharibu kiwango chake.
Kocha wa Al Saad anamtaka kiungo huyo akaungane na kiungo mwingine wa Kihispania Santi Carzola katika safu ya kiungo ya klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Rodriguez alifanya vizuri katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 kwa kuibuka kuwa mfungaji bora wa michuano,baada ya michuano hiyo alijiunga na Real Madrid.Baadaye alitolewa kwa mkopo Bayern Munich kabla ya kuuzwa Everton mwaka 2020.