Sports Leo

Jezi Yanga Sc Zawashika Mashabiki

Klabu ya Yanga SC imezindua jezi zake mpya kwa msimu wa 2025/26, na kama kawaida mashabiki hawakubaki kimya  katika mitaa yote jijini Dar es Salaam mpaka Mwanza kumejaa kijani, njano na nyeusi. Hizi ndizo jezi zitakazotumika kwenye Ligi Kuu ya NBC na michuano ya kimataifa ambapo Wananchi wanategemea kupenya mbali zaidi.

Aina Tatu, Historia Moja

Kwa mujibu wa tamaduni za tangu mwaka 1935, kijani imebaki kuwa rangi ya nyumbani, njano ya ugenini, na nyeusi ikiwa jezi ya tatu. Ukiziona, unajua moja kwa moja hii ni Yanga ambapo watabadili jezi hizo kutokana na muktadha wa mchezo wenyewe huku ile nyeusi ikiwa kama jezi mbadala pindi njano na kijani zikiwa hazitumiki,hiyo siyo mchezo!

Jezi Mpya za Yanga SC 2025/2026 - sportsleo.co.tz

Katika jezo hizo,kifuani kumevalishwa nembo ya SportPesa, huku nakshi na urembo wa jezi mpya zikipeleka mashabiki mbali. Hii si jezi ya kuvaa uwanjani pekee, hata mitaani zinaingia kama fashion kali hasa kwa mabinti na mabishoo wa mjini ambao hujua kupangilia mavazi kwa ufasaha na unadhifu zaidi.

Mashabiki Wazipokea Kwa Shangwe

Hata kabla jasho halijakauka kwenye uzinduzi, maelfu ya mashabiki walikuwa tayari wanazipata sokoni. Jezi ya njano imeonekana kufanya “kolabo na mitaa” ambapo kila kona imejaa watu wakipiga picha, wengine wakipanga foleni madukani. Mmoja aliandika mtandaoni “Hii njano ikipigwa na suruali nyeusi, hata ukikutana na Simba barabarani anakukwepa mwenyewe.”Alisema shabiki huyo akiwa katika muundo wa utani wa jadi.

Utani wa Jadi Umeamka Vijiweni na mitaani

Mara baada ya uzinduzi, mashabiki wa Simba hawakukaa kimya huku wengine wakisikika wakisema, “hizi njano zitaishia mbugani tu, Ligi ya Mabingwa haitaziona”. Lakini mashabiki wa Yanga wakajibu kwa tambo na majivuno mengi “Mbugani tunavuna pointi, Ulaya tunavuna exposure” jezi zetu zipo kimataifa, zenu bado zinaonekana kama sare za shule.”Alijibu mama mmoja mbele ya mashabiki lukuki wa Simba sc.

Hapo ndipo moto wa jadi uliwaka zaidi, kila upande ukijigamba  lakini ukweli unabaki kwamba jezi mpya za Yanga zimeleta hamasa ya aina yake ambapo wananchi wamepiga hatua nyingine kutoka kwa Sheria Ngowi Hadi Ubunifu Mpya ambapo kwa takribani wa misimu mitatu, Yanga ilitumia ubunifu wa Sheria Ngowi, lakini safari hii wametoka na ladha mpya huku mashabiki na wadau wa soka nchini wakiwa wanakubaliana: ubunifu huu ni level nyingine kabisa.

Kwa mashabiki wa soka Tanzania, jezi si vazi la kawaida – ni heshima, ni historia, na ni utambulisho. Jezi mpya za Yanga SC msimu huu zimeleta msisimko mkubwa, zimechochea utani wa jadi, na bila shaka zimezidi kuimarisha hadhi ya klabu hiyo kama bingwa wa mavazi na historia.

Exit mobile version