Home Soka JKT Vs Yanga sc Kupigwa Leo

JKT Vs Yanga sc Kupigwa Leo

by Sports Leo
0 comments

Mechi kati ya JKT na Yanga Sc iliyoahirishwa jana Aprili 23, 2024 itapigwa leo Aprili 24 kuanzia saa 10:00 kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam kutokana na ratiba mpya ya bodi ya ligi kuu nchini.

Mchezo huo awali ulishindikana kuchezwa hapo jana kutokana na uwanja huo kujaa maji kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha jijini Dar es salaam na maeneo ya jirani ambapo sehemu kubwa ya uwanja ilikua na maji na matope.

Baada ya mchezo huo kuahirishwa sasa utachezwa leo jioni ambapo Yanga sc itakua mgeni wa Jkt Tanzania ambao wamegoma kuhamishia mchezo huo katika uwanja wa Azam Complex ama mahali kwingine ambapo kimsingi kwa mujibu wa kanuni wako sawa kama timu mwenyeji.

banner

Yanga sc mpaka sasa ana alama 58 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ambapo akishinda atafikisha alama 61 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo huku Jkt Tanzania wakiwa katika nafasi ya 15 na alama 22 katika michezo 22 ya ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited