Home Soka Kadi Ya Son Yafutwa

Kadi Ya Son Yafutwa

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka la nchini Uingereza(Fa) limeifuta kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa timu ya Tottenham Hotspurs Son Heung-min baada ya kujiridhisha kuwa kuwa mchezaji huyo hakumgusa mchezaji wa Everton Andre Gomes katika tukio lililosababisha staa huyo kuvunjika mguu.

Adhabu hiyo imefutwa baada ya klabu ya Tottenham kukata rufaa kufuatia kadi hiyo ambayo ingemlazimu staa huyo kukaa nje akitumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.

Faulo hiyo ilimuweka matatani kiungo huyo wa Everton baada ya kuvunjika mguu ambao ameshafanyiwa operasheni ambayo imekua na mafanikio makubwa japo atalazimika kukaa hospitali kwa wiki kadhaa.

banner

Picha za video zimeonyesha Son kutomgusa staa huyo na bali Serge Aurier ndie aliemkanyaga na kumvunja mguu na tayari Son ameshafanyiwa matibabu ya kisaikolojia ili aweze kucheza mechi zijazo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited