Wachezaji Francis Kahata na kipa Farouk Shikhalo wameibuka wachezaji bora wa kombe la Mapinduzi cup lililomalizika visiwani Zanzibar.
Kahata ambaye kwenye michezo ya ligi amekua hapati nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza amecheza michezo yote katika kombe la mapinduzi na kuibuka mchezaji bora wa michuano hiyo huku Farouk Shikhalo akiibuka kipa bora baada ya kuonyesha umahiri wa kutosha hasa katika kuokoa michomo ya penati.
Miraji Athuman ameibuka mfungaji bora wa michuano akifunga mabao manne huku Joash Onyango akiibuka mchezaji bora wa mechi ya fainali.