Vinara wa Ligi Kuu, Simba wanaendelea kuimarisha kikosi chao kwa kuwaongeza mikataba wachezaji ambao mwisho wa msimu huu unamalizika.
Jana Juni 7, walimazana na kipa wao namba mbili, Beno Kakolanya katika suala la kumuongeza mkataba mpya wa miaka miwili kwani ule wa awali unamalizika mwisho wa msimu huu.
Simba walimsajili Kakolanya kutokea Yanga 2019-20, kwa mkataba wa miaka miwili ambao mwisho wa msimu huu ulikuwa unamalizika huku kocha wa makipa wa klabu hiyo akisisitiza kuwa anahitaji kusalia na makipa wote watatu waliopo klabuni hapo hivyo kurahisisha zoezi la kumuongezea mkataba kipa huyo.