Site icon Sports Leo

Kambole Aiwekea Ngumu Yanga sc

Klabu ya Yanga sc ipo mbioni kuachana na dili la kumsajili mshambuliaji Razalus Kambole kutokana na mchezaji huyo kudai kiwango kikubwa cha mshahara wa kila mwezi.

Awali Yanga sc ilishakubaliana na klabu ya Kaizer Chiefs kuhusu kumsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja huku wakiambia wakubaliane maslahi binafsi na mchezaji ambapo mchezaji alidai mshahara wa dola elfu kumi kwa mwezi kitu ambapo mabosi wa klabu hiyo hawakukubaliana nacho ikizingatiwa kuwa mchezaji alikua hachezi kwa muda mrefu.

Inadaiwa kuwa mabosi wa Yanga sc wanahitaji mshahara usiozidi dola elfu tano tu ili kutoharibu viwangi vya mishahara kwa mastaa mbalimbali klabuni hapo.

Exit mobile version