Kiungo Ngolo Kante alikua kikwazo kwa Real Madrid kuibuka na ushindi mbele ya Chelsea katika mchezo wa nusu fainali klabu bingwa barani ulaya uliofanyika nchini Hispania.
Kiungo huyo aliwadhibiti ipasavyo viungo wa Real Madrid wakiongwa na Ton Kroos na Casemiro kiasi cha kushindwa kuipeleka timu juu na kusababisha bao la uongozi kwa Chelsea kupitia kwa Christian Pullisic dakika ya 14 huku Madrid wakisawazisha robo saa baadae kwa kiki ya Karim Benzema kufuatia pasi ya Elder Militao.
Kazi kubwa iliyofanywa na Kante ilimfanya Pullisic kuwa huru muda nwingi kiasi cha kuweka rekodi ya kuwa Mmarekani wa kwanza kufunga goli hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo huku Madrid wakipiga mashuti machache zaidi yaliyolenga lango tangu msimu wa 2003-2004.