Site icon Sports Leo

Kaseke Aipeleka Yanga sc Nusu Fainali

Mabao mawili yaliyofungwa na Deus Kaseke dakika za 26 na 56 yameipeleka klabu ya Yanga sc hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Azam Tv.

Yanga sc baada ya kuipiga Mwadui Fc sasa itasafiri mpaka mkoani Mara ambapo itawavaa Biashara United anbayo imefanikiwa kuifunga Namungo Fc mabao 2-0 hapo jana.

Kesho ni zamu ya mabingwa watetezi wa taji hilo Simba kusaka nafasi ya kushiriki nusu fainali ambapo itamenayna na Dodoma Jiji.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa ambapo utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Exit mobile version