Kocha wa Young Africans SC ya Dar es Salaam, Cedric Kaze amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2020/21, huku Saido Ntibazonkiza wa Young Africans pia akichaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi huo.
Saido na Kaze walitwaa tuzo hizo baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao fainali kwa mwezi Disemba katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo za VPL, kutokana na mapendekezo ya makocha waliopo vituo mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.
Kwa Disemba, Saido aliwashinda kiungo Clatous Chama wa Simba na kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji FC, Seif Karihe alioingia nao fainali huku Kaze akiwashinda Sven Vandenbroeck wa Simba na Francis Baraza wa Biashara United.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga chini ya Kaze kwa mwezi huo ilishinda michezo minne na kutoka sare mmoja ikivuna pointi 13 na kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi. Yanga ilizifunga Ruvu Shooting FC (2-1), Mwadui FC (0-5), Dodoma Jiji FC (3-1) na Ihefu SC 0-3 huku wakitoka sare na Tanzania Prisons FC 1-1.