Mchezaji kinda wa Kitanzania Kevin John maarufu kama ”Mbappe” amejiunga rasmi na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji akitokea katika akademi ya klabu ya Leicester ya nchini England alikokua akisoma na kupata mafunzo ya soka.
Mchezaji huyo ametambulishwa rasmi na klabu hiyo ya Ubelgiji baada ya kufikisha miaka 18 inayomruhusu kusajiliwa kama mchezaji wa kulipwa na atajiunga moja kwa moja na timu ya wakubwa tofauti na ilivyoripotiwa awali kuwa angejiunga na timu ya vijana ya Genk.
Katika taarifa ya klabu hiyo imemshukuru Mbwana Samatta kwa kuwapa vidokezo kuhusu kinda huyo ikimtaja kama kama kijana imara na mwenye kasi akisaini hadi mwaka 2024.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.