Sports Leo

Kibu,Kibwana waongezwa Stars

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen amewaongeza kikosini mshambuliaji wa Simba Sc Kibu Denis na beki wa Yanga Sc Kibwana Shomari katika kikosi hicho.

Kim alionesha kumhitaji sana Kibu Denis kiasi cha kupelekea TFF kumuombea uraia mchezaji huyo kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo alipewa uraia wa Tanzania Septemba 30.

Kwa upande wa Kibwana ambaye amekuwa katika kiwango kizuri tangu ajiunge na Yanga msimu uliopita hatimaye amepata nafasi aliyostahili mara baada ya wadau wa soka nchini kuhoji kwanini hajumuishwi ndani ya kikosi hicho,na huenda akawa mbadala wa Shomari Kapombe ambae alipata majeraha kidogo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United.

Taifa Stars itakabiliana na Benin siku ya Alhamisi katika mchezo wa tatu wa kufuzu kombe la dunia Qatar 2022 kabla ya kurudiana nao tena Oktoba 10 ugenini,wakati huo huo kiungo Jonas Mkude ameomba kuondolewa kwenye kikosi hicho kutokana na sababu za kifamilia na ameruhusiwa na kocha Kim.

Exit mobile version