Home Soka Kinda la Barca Lageuka Lulu Hispania

Kinda la Barca Lageuka Lulu Hispania

by Sports Leo
0 comments

Kinda wa timu ya Barcelona Ansumane “Ansu” Fati amegeuka lulu baada ya shirikisho la soka nchini humo kuanza harakati za kumpatia uraia ili aje achezee timu ya taifa ya nchi hiyo.

Shhirikisho hilo la soka la nchi hiyo limelazimika kuanzisha mchakato huo mapema ili lianze kumtumia kinda huyo mwenye miaka 16 katika ngazi za timu za vijana ili kumshawishi achezee taifa hilo badala ya nchi aliyozaliwa ya Guinnea Bissau.

Ansu amekua maarufu hivi karibuni baada ya kuwa kinda mdogo zaidi kucheza ligi hiyo akivunja rekodi iliyowekwa na Vicenc Martinez baada ya kucheza mchezo wa ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Real Betis ambapo kinda huyo aliingia dakika za mwisho.

banner

August 31 mwaka huu ni siku ya kukumbukwa kwa kinda huyo alipofunga dhidi ya Osasuna katika mchezo wa ligi kuu kabla ya kufunga na kusaidia upatikanaji wa bao katika mchezo wa jumamosi iliyopita dhidi ya Valencia.Barcelona wana mkataba na kinda huyo mpaka 2022 na wameweka kipengele cha paundi milioni 100 kwa timu itakayomhitaji.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited