Home Soka Kisa Simba Sc,Mosimame Kikaangoni Misri

Kisa Simba Sc,Mosimame Kikaangoni Misri

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha wa klabu ya Al ahly Pitso Mosimane yuko kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa wachezaji wa zamani wa Al ahly, mashabiki na wadau wengine baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba sc uliofanyika siku ya jumatano jijini Dar es salaam.
Golikipa wa zamani wa Al ahly Ahmed Shobier ambaye ni mchambuzi mkubwa Egypt na mwenye ushawishi kwenye klabu hiyo bingwa wa muda wote wa Africa amemlaumu sana Pitso Mosimane baada ya kupoteza mchezo huo.
Kipa huyo amesema Al ahly  imecheza vibaya sana kuliko wakati wowote tangu ianzishwe kwenye mchezo dhidi ya klabu ya Simba sc huku akisisitiza  Al ahly sio ya kuiogopa Simba bali Simba ndio inapaswa kuiogopa Al ahly.
Ameeleza kwamba ushindi wa As Vita umeongeza shinikizo kwenye kundi hivyo Mosimane anawakati mgumu sana endapo hata pata alama  kwenye mchezo dhidi ya klabu ya As vita ya Dr Congo.
“Nina mashaka na Pitso Mosimane, asisingizie hali ya hewa, timu imecheza ovyo sana, sub zake pia hazieleweki, timu imecheza chini sana na slow”alisema kipa huyo
Chanzo:Tomcruz

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited