114
Winga teleza wa Klabu ya Yanga Tuisila Kisinda ‘TK Master” amesema kwa sasa yuko sawa kabisa kiafya na kimchezo, na anaendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mechi ngumu hapo kesho dhidi ya Simba SC lakini kwa sasa hana presha yoyote kuelekea mchezo huo.
Kisinda amesema mechi ya kwanza waliyokutana katika mzunguko wa Kwanza dhidi ya Simba SC, kidogo ndio iliyomfanya kuwa na presha sababu alikuwa hajui ni mechi ya aina gani, lakini mchezo huu hautakuwa na presha yoyote kwake, muhimu ni kuwa katika ubora wake ili aweze kuisaidia timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi.
Kisinda aliongeza kuwa ana shauku ya kucheza mechi kubwa kama hizo ambazo zimekuwa zikimtambulisha zaidi makali yake, sababu hata kipindi yuko DR Congo walimfahamu pindi walipokuwa wanakutana na TP Mazembe huwa anapenda kung’aa katika mechi za namna hiyo, hivyo anataka kufanya kazi kubwa zaidi katika mechi ya kesho kuliko alivyocheza mechi mbili zilizopita.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.