Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga sc Rafael Daud Loth amejiunga na klabu ya Ihefu Fc miezi sita baada ya usajili wake wa awali kujiunga na Mwadui Fc kukwama.
Daud ni mmoja ya viungo washambuliaji wazoefu huku wakiwa na kimo kizuri kuweza kuhimili mikiki ya viwanjani ambapo aling’ara zaidi akiwa na Yanga sc aliyojiunga nayo msimu wa 2017 akicheza kwa muda wa miaka miwili.
Loth ataisaidia Ihefu ambayo imekua na matokeo yasiyoridhisha kiasi cha kutishia uhai wake katika ligi kuu nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.