Kikosi cha KMC FC kimerejea jijini Dar es Salaam leo kikitokea mkoani Tanga ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana dhidi ya Coast Union uliopigwa katika uwanja wa Mkwakwani na kumalizika kwa sare ya kutokufungana.
KMC FC imerejea Jijini Dar es Salaam ambapo kesho itaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo mwingine wa Ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting mchezo utakao chezwa katika uwanja wa Uhuru saa 16: 00 mchana.
KMC FC iliondoka Jijini Dar es Salaa, Machi mbili ambapo iliwasili Jijini Arusha na kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Machi Nne katika uwanja wa Sheih Amri Abeid dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliomalizika kwa Kino Boys kupoteza kwa kufungwa goli moja kwa bila.
Nb:Imetolewa na Afisa Habari Wa Kmc Fc Christina Mwagala
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.