Site icon Sports Leo

Kocha Yanga Awasili

Kocha mkuu wa Yanga LUC EYMAEL tayari ameshawasili nchini Tanzania kuja kuendelea na majukumu yake katika klabu hiyo ambapo kesho ataelekea Shinyanga kuungana na kikosi chake cha Young Africans tayari kwa mapambano ya kumaliza ligi kuu.

Kocha huyo ataungana na timu hiyo huku kukiwa na mpango mkakati wa kuhakikisha Yanga inachukua kombe la FA na inamaliza nafasi ya pili katika ligi kuu nchini.

Kurejea kwa kocha huyo kumemaliza sintofahamu ya muda mrefu iliyojitokeza hapo awali kuhusu kuwasili kwa kocha huyo maarufu nchini.

Exit mobile version