Home Soka Kocha Yanga sc Amtetea Shikhalo

Kocha Yanga sc Amtetea Shikhalo

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa makipa wa klabu ya Yanga Razack Siwa amesema goli walililofungwa Yanga sc na Prince Dube wa Azam fc kipa Farouk Shikhalo hapaswi kulaumiwa kwani mpigaji alitumia ujuzi na akili na kufungwa haikua uzembe wa kipa.
“Mpigaji alitumia ujuzi na alitumia akili ya kufunga, kufungwa haikuwa uzembe wa kipa wetu kwa sababu hata sisi tuliweza kupata nafasi waliyopata Azam FC kwa kupiga shuti la mbali na kushindwa kutumia vizuri nafasi,”.
“Tulitengeneza nafasi nyingi hatukuweza kutumia kwa sababu hatukuwa watulivu ila wenzetu walipata umakini na utulivu mkubwa wa kupata ushindi huo,” alisema Razak Siwa.

 

Yanga sc imepoteza mchezo wa pili baada ya kukubali kipigo cha bao moja dhidi ya Azam Fc mchezo uliofanyika siku ya jumapili Aprili 25 uwanja wa Mkapa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited